30 May
30May

Katika mapambano ya kutetea watoto wa kike wenye kunyimwa fursa za kusoma na kutimiza ndoto zao MOMEC production ikaamua kuja na moja kati ya hadithi zake za kweli zilizowahi kutokea miongoni mwa mabinti wadogo katika ulimwengu huu wa sasa wa sayansi na teknolojia na ni ulimwengu wa kupiga vita ukiritimba unyanyasaji wa kijinsia katika kuielemisha jamii ndipo wakatengeneza movie iitwayo SAUTI YA KUNESE movie hii imefanyiwa mkoani shinyanga lengo la movie hii ni kutaka kuielimisha jamii kuwa bado mtoto wa kike anathamani na kama atapewa haki zake zote anaweza na kama ilivyokuwa hapo awali mtoto wa kike alikuwa ni wa kukaa nyumbani na kuangalia majukumu ya ndoa.... katika story hii ya Sauti ya kunese utapata kuona binti anaeozeshwa kwa lazima akiwa na umri mdogo lakin pia utapata kuona madhara ya ndoa hiyo ya utotoni lakini pia hatima kwa serikali juu ya kupiga vita ndoa za utotoni na ujane katika umri mdogo ni vyema tukawapa msaada watoto wa kike kusoma na kutimiza malengo yao kwani ni gharama ndogo sana kumsomesha mtoto wa kike akajimudu kuriko kumpa mume akiwa mdogo mwisho atarudi nyumbani akiwa mgonjwa lakini pia ni mwenye watoto wengi asioweza kuwamudu katika malezi hivyo kupelekea umasikini kuongezeka katika jamii ya kiafrika kwa pamoja tuseme........KOMESHA NDOA ZA UTOTONI NA ZUIA UJANE KWA MTOTO MDOGO............by Muhammad Amir Kibinda editor and Camera man MOMEC PRODUCTION

Maoni
* Barua pepe haitachapishwa kwenye wavuti.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING